Tetesi za usajili yanga 2025 26 dirisha kubwa

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga SC, wameanza kuonesha nia yao ya dhati ya kuimarisha kikosi chao kuelekea msimu mpya wa 2025/2026. Hatua hii inakuja kufuatia baadhi ya wachezaji wao tegemezi kuondoka klabuni hapo, hali iliyoibua haja ya kufanya usajili wa kimkakati ili kuhakikisha ushindani unaendelea kudumu katika mashindano ya kitaifa na kimataifa, ikiwemo Ligi Kuu ya NBC, Kombe la Shirikisho la CRDB, na michuano ya CAF.

Katika kipindi hiki cha dirisha la usajili, tetesi za usajili Yanga leo 2025/2026 zimechukua nafasi kubwa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Taarifa zinaonesha kuwa Yanga SC imejikita katika kuhakikisha kikosi kinakuwa bora zaidi kwa kuwasajili wachezaji wa ndani na wa kimataifa wenye uwezo wa juu, nidhamu, na uzoefu unaohitajika kwenye soka la ushindani.

Wachezaji Walioongeza Mikataba Yanga

Maxi Nzengeli

Mshambuliaji wa DR Congo, Nzengeli, ameendelea kuwa mchezaji wa kuaminika kwa ubora wake wa kucheza nafasi mbalimbali. Msimu huu amefunga mabao 5 na kutoa asisti 7. Tayari ameongeza mkataba hadi 2027 licha ya kukumbwa na majeraha awali.

Pacome Zouzoua

Mchezaji wa Ivory Coast aliyefanya kazi kubwa kwenye eneo la ushambuliaji msimu huu, akiwa na mabao 7 na asisti 8 katika mechi 24. Ametajwa tayari kuafikiana kuongeza mkataba hadi 2027.

Dickson Job

Nahodha msaidizi na beki tegemezi wa Stars, ameongeza mkataba hadi 2027 licha ya Simba SC kuonyesha nia ya kumsajili.

Mudathir Yahya

Kiungo wa Tanzania aliyedhihirisha uwezo wake msimu huu licha ya kuanza akiwa si chaguo la kwanza. Azam FC inahusishwa naye, lakini Yanga bado inataka kumbakiza

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *