Kuziba Jino ni huduma ya Kuweka dawa maalumu kwenye jino lililo tobolewa na wadudu ambao wanapatikana kwenye kinywa.

Tabibu anaweza kuziba dawa ya mda mfupi au mda mrefu kulingana na kina cha jino kilivyotobolewa. Mfano wa dawa ya mda mfupi ni Zinc Oxide Eugenal(ZOE) ambayo husaidia kutuliza maumivu,ina uzani sawa wa pH hivyo upelekea kua rafiki na fizi iliyopo karibu na jino,kuweza kulinda jino dhidi ya vyakula na wadudu wasiweze kuingia kwenye jino husika na kuweza kushambulia kwa mara nyingine tena.

Dawa ya mda mfupi

Dawa hii ya mda mfupi mara nyingi hudumu ndani ya mwezi mmoja tu maana huwa inatoka(kugaduka gaduka) taratibu kadri ya mda unavyokwenda. Pia harufu yake inakua si rafiki kwa baadhi ya watu

Mfano wa dawa za mda mrefu ambazo zinauwezekano wa kupatikana kwa urahisi ni Glass Ionomer cement(GIC), Composite material na Amalgam

1. Glass Ionomer cement(GIC)

Hii ni dawa ya mda mrefu ambayo hutumika kwa jino ambalo halija chimbika sana(kukaribia kwenye mzizi wa jino). Hutumika kushikiza kichwa cha jino bandia(Crown & Bridge) na pia kuziba mifereji mikubwa ya meno hasa kwa meno ya nyuma(Fissure sealing).

Glass ionomer cement

Uzuri wa hii dawa tabibu huchagulia kulingana na namna ya jino lilivyotoboka na huzingatia rangi ya jino husika.

2. Composite Material

Ni aina ya dawa yakuzibia kwa mda mrefu ambayo haswa hutumika kwa meno ya mbele. Hii ni kwasababu ya uchaguzi wa mfanano Sahihi wa rangi ya dawa na rangi ya jino. Pia ni rahisi kwa tabibu kuunda umbo lolote lenye mfanano na meno mengine.

Dental composite material

Kuna aina mbalimbali za dawa hii ya kuzibia meno, tabibu huchagua kulingana na aina ya kazi na kina cha jino husika. Mfano Floweble composite material hutumika kwa jino lililo tobolewa kwa kina kidogo na kwa jino lenye kina kirefu hutumika kama kianzio cha dawa. Macro & Microfilled composite hii ni aina ya dawa ambayo hutumika mara nyingi kwasababu ya uwezo wake wa kunyumbulika,laini na hutoa muonekano ang’avu wa jino. Hizi ni aina chache tu za dawa hii,zimechaguliwa kwasababu ndizo hutumika zaidi.

3. Dental Amalgam

Ni dawa ya kuzibia meno kwa mda mrefu yenye mchanganyiko wa 50% ya kimiminika cha mercury na unga wa silver,tin au Copper. Dawa hii ina sifa ya kua imara(ngumu) zaidi na inayodumu kwa mda mrefu zaidi.

Dental Amalgam

Licha ya faida ya kua na uimara zaidi lakini ni dawa inasadikika kua ilitumika miaka ya nyuma zaidi na uwepo wa kimiminika cha mercury inafanya isiwe chaguo bora kwasababu za kiafya, vilevile hata muonekano wake sio rafiki kwa walio wengi kwa kua muonekano wake hua silver(mweusi). Dawa hii pia hupitisha joto,kama tabibu hatoweza kuziba kwa umaridadi basi mgonjwa anaweza kupata changamoto hasa akiwa anatumia kitu cha joto/moto.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Explore More

Dental Implants

Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry. Lorem Ipsum has been the industrys standard dummy text ever since the 1500s, when an unknown printer took

Dental Filling

Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry. Lorem Ipsum has been the industrys standard dummy text ever since the 1500s, when an unknown printer took

Dental Orthodontics

Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry. Lorem Ipsum has been the industrys standard dummy text ever since the 1500s, when an unknown printer took